Usawiri wa Mzazi wa Kiume Katika Fasihi ya Watoto

Abstract
Fasihi ya watoto ina changia kwa upana katika kukuza ufahamu kuhusu familia na malezi. Mchango wa kina mama katika familia umehusishwa zaidi kwenye kazi nyingi za fasihi. Nafasi ya mzazi wa kiume inaendelea kukua huku akijadiliwa kwa njia changamano. Zipo kazi zinazomsawiri mzazi huyu kama baba anayehusika kikamilifu ilhali kazi nyingine zinamchora kama mzazi anayetoweka majukumu yake. Makala haya yatachunguza nafasi aliyopewa mzazi wa kiume katika kazi za fasihi zilizoandikwa katika karne ya ishirini na moja. Aidha kwa kufafanua nafasi ya mzazi wa kiume, hisia za watoto kuhusu kina baba zitaeleweka. Kwa kuchunguza mchango wa kina baba makala haya yatawaongoza waandishi wa kazi za fasihi kuhusisha mzazi wa kiume kikamilifu, katika malezi bila kutegemea wazazi wa kike tu. Makala haya yanashikilia kauli kuwa mzazi wa kiume ni mzazi tosha anayefaa kuwatimizia watoto majukumu yote kikamilifu. Aidha, makala haya yanapinga dhana kuwa malezi bora, yenye mapenzi na hisia ni ya mama tu. Makala haya yataegemea nadharia ya ujifunzaji wa kijamii iliyoasisiwa na Albert Bandura. Kulingana na nadharia hii mtoto huweza kupata na kuiga tabia zilizo katika mazingira yake. Mazingira haya yanaweza pia kuhusisha wahusika waliosawiriwa kwenye vitabu wanavyovisoma. Iwapo wazazi wa kiume wataumbwa katika kazi za fasihi wakiwa kielelezo chema, wakiwa na sifa chanya na mfano wa kuigwa, basi watoto watajifunza kuwa na tabia njema na watajivunia kuhusishwa na kina baba. Utafiti huu utafanyiwa maktabani baada ya kusoma novela teule, na utawasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo yake yafafanua mifumo mbalimbali ya nafasi za kina baba katika fasihi ya watoto.
Cite this Item
Njuguna, L., Maitaria, J., & Kinyanjui, P. (2026). Usawiri wa Mzazi wa Kiume Katika Fasihi ya Watoto. East African  Nature &  Science  Organization. https://karuspace.karu.ac.ke/handle/20.500.12092/3596

Description

Usawiri wa Mzazi wa Kiume Katika Fasihi

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

East African Nature & Science Organization

Usage Metrics

2 Views
10 Downloads