Malezi ya Mtoto wa Karne ya Ishirini na Moja Katika Novela za Assumpta K. Matei
Abstract
Makala hii inachunguza namna malezi ya mtoto wa karne ya ishirini na moja yanavyowasilishwa katika novela tatu za Assumpta K. Matei: Mji wa Matarajio (2022), Uteuzi wa Chale (2022) na Tumaini la Mzeituni (2025). Ingawa tafiti zilizotangulia zimejadili malezi, usawiri wa watoto, teknolojia na masuala ibuka katika fasihi ya watoto, bado hazijaeleza kwa kina namna mabadiliko ya kiuchumi, kiafya, kimazingira na kiteknolojia yanavyobadili mahitaji, majukumu ya walezi na mahusiano ya kimalezi katika novela za Matei. Utafiti ulitumia mkabala wa kiubora, muundo wa kimaelezo kiuchanganuzi, usomaji wa karibu na uchanganuzi wa nyaraka. Data ilichanganuliwa kimaudhui kwa kuzingatia Nadharia ya Uhalisia wa Kijamii. Matokeo yanaonyesha kuwa umaskini katika Mji wa Matarajio unafanya elimu, ulinzi wa mtoto na msaada wa kihisia kuwa changamoto katika malezi; ugonjwa katika Uteuzi wa Chale unapanua wigo wa malezi kujumuisha afya, mwendelezo wa elimu, ustawi wa kihisia na ukuzaji wa kipaji; huku mafuriko katika Tumaini la Mzeituni yakifanya usalama, uhamaji, elimu na ustahimilivu kuwa sehemu muhimu za malezi. Aidha, sauti ya mtoto na ushirikiano wa familia, rika na taasisi huwezesha malezi kukidhi mahitaji yanayotokana na mazingira yanayobadilika. Utafiti unahitimisha kuwa Matei anawasilisha malezi kama mchakato shirikishi na jumuishi. Utafiti huu ni muhimu kwa sababu unaonyesha namna fasihi ya watoto inavyoweza kuchangia malezi yanayozingatia haki, ustawi na mahitaji yanayobadilika ya mtoto wa karne ya ishirini na moja. Utafiti unapendekeza matumizi ya fasihi ya watoto katika kuhamasisha malezi yanayozingatia haki, ustawi na ujumuishaji.
Cite this Item
Description
mtoto wa karne ya ishirini na moja
Download Files
Date
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Eastern Africa Journal of Kiswahili
Usage Metrics
0 Views
3 Downloads
