Show simple item record

dc.contributor.authorMWANIKI, MILKAH WANJUGU
dc.date.accessioned2023-11-28T13:38:40Z
dc.date.available2023-11-28T13:38:40Z
dc.date.issued2023-11
dc.identifier.urihttps://karuspace.karu.ac.ke/handle/20.500.12092/3008
dc.descriptionTASNIFU HII IMETOLEWA ILI KUTOSHELEZA BAADHI YA MAHITAJI YA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA CHUO KIKUU CHA KARATINAen_US
dc.description.abstractKinaya ni mbinu muhimu ya kimtindo ambayo hutumiwa na waandishi wa riwaya na watunzi wa tamthilia kuwasilisha ujumbe wao katika kazi za fasihi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa: Kuchunguza matumizi ya kinaya kama mbinu ya kimtindo katika kubainisha maudhui na wahusika katika matini mbili za fasihi ya Kiswahili ambazo ni: riwaya ya Assumpta K. Matei ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo ya Pauline Kea. Malengo ya utafiti yalikuwa; moja, kubainisha aina mbalimbali za kinaya katika kazi teule za fasihi; mbili, kueleza jinsi kinaya kimetumika kuendeleza maudhui katika matini mbili teule za fasihi ya Kiswahili; tatu, kueleza jinsi kinaya kinavyotumika katika kujenga sifa za wahusika katika kazi teule. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Kimtindo pamoja na mihimili yake ambayo iliongoza kila sura ya utafiti huu. Nadharia hii inaeleza kwamba ili kuielewa kazi ya fasihi, msomaji anafaa kuelewa kuhusu mbinu za lugha ambazo zimetumika. Utafiti huu unaangazia mbinu ya kinaya vile imetumika katika kubainisha maudhui kama vile uongozi mbaya, ukatili, unafiki na ufisadi. Miongoni mwa waasisi wake ni Coombes (1953). Riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo ziliteuliwa kimakusudi kwa msingi wa utajiri wao wa kinaya. Ili kupata data katika utafiti, mtafiti alisoma vitabu, nadharia, na majarida yanayohusiana na mada ya utafiti. Utafiti ulitumia muundo wa utafiti wa kimaelezo. Mjadala wa vikundi lengwa uliohusisha washiriki wanne pamoja na mtafiti ulitumika kukusanya data kutoka katika matini teule. Data ilichanganuliwa kwa misingi ya malengo ya utafiti. Utafiti unabainisha kuwa kuna aina mbalimbali za kinaya katika kazi za fasihi. Hizi ni: Hali, drama, mazungumzo, kilimwengu, na kinaya cha kisokratiki. Utafiti pia unadhihirisha kuwa vinaya vya hali, mazungumzo na drama ndizo msingi katika ukuzaji wa dhamira na wahusika katika matini mbili teule. Utafiti huu ulihitimisha kuwa kinaya huwa muhimu katika fasihi kwa kuwa hutumika katika kubainisha maudhui hasi katika jamiii kwa kuonyesha matendo maovu ya wahusika wanayotenda kinyume cha matarajio ya wahusika wengine. Kwa mfano viongozi wanaweza kujitokeza wakitenda matendo hasi kama vile mauaji, usaliti uzinzi na ubinafsi kinyume na matarajio ya wananchi waliowateua.Tena kinaya ni muhimu kwa kuwa hutumiwa kueleza sifa za wahusika katika fasihi kwa kuonyesha vile wahusika wanatenda maovu jambo ambalo ni kinyume cha matarajio ya wahusika wengine na pia wasomaji.kuwasilisha maudhui na wahusika katika kazi za fasihi na kinapaswa kufasiriwa kimuktadha ili kuimarisha mawasiliano. Utafiti unapendekeza kuwa watafiti wa lugha watumie kinaya kama nyenzo ya kuwasilisha masuala yanayodhihirika katika jamii. Utafiti huu unanuiwa kuwanufaisha watafiti wa fasihi ya Kiswahili, wanafunzi, waandishi wa riwaya na watunzi wa tamthilia ili kubainisha dhima ya mitindo ya kifasihi kama vile kinaya katika kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa na mwandishi.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKaratina Universityen_US
dc.titleKINAYA KAMA NJIA YA KUBAINISHA MAUDHUI: MIFANO KUTOKA RIWAYA YA CHOZI LA HERI NA TAMTHILIA YA KIGOGOen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record