• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Research Publications
    • School of Education and Social sciences
    • Department of Humanities and Languages
    • View Item
    •   Repository Home
    • Research Publications
    • School of Education and Social sciences
    • Department of Humanities and Languages
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Dhima ya Ushairi wa Kiswahili Katika Kuelimishia Jamii Kuhusu Demokrasia

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (268.9Kb)
    Date
    2014
    Author
    Maitaria, Joseph Nyehita
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Makala haya yanafafanua dhima ya Ushairi wa Kiswahili katika kubainisha na kuielimishia jamii kuhusu masuala ya demokrasia. Ushairi kama kitengo muhimu cha fasihi, umekuwa ukitumiwa kuchochea usaili na tafakari kuhusu uhusika wa watu katika uongozi wa jamii. Aidha, umaarufu wake hautokani tu na maneno ya lugha iliyozoewa katika jamii bali kupitia kwa tamathali za usemi ambazo huhusishwa kwa makusudi katika ubebaji wa ujumbe unaowasilishwa.Hivyo, utanzu huu unakuwa ni nyenzo ya kuwaelekeza, kuwaelimisha na kuwazindua watu kuhusu uwajibikaji wa kushiriki na kuchangia kwa dhati katika masuala ya siasa na uongozi wa jamii. Katika miaka ya mwanzo mwanzo mwa 1960 hadi miaka ya 1990, serikali za mataifa ya Afrika Mashariki zimekuwa zikijitahidi kwa kiwango fulani lakini hazijaudhibiti mwafaka wa kuhusisha umma katika masuala muhimu ya kitaifa. Kutokana na mabadiliko asasi za jamii ya sasa, kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti kuhusu falsafa na matarajio ya watu kuhusu uelekezaji wa maisha yao. Baadhi ya wanajamii wamekuwa wakisaili na kukemea baadhi ya vitendo hasi vinavyoshuhudiwa katika mfumo wa utawala uliopo katika jamii. Kadhalika, ushairi wa Kiswahili umekuwa ukiyabainisha na kuyafakari baadhi ya masuala hayo kwa jicho pekuzi. Kwa maana hii, suala la demokrasia linashughulikiwa katika makala haya kwa kurejelea baadhi ya mashairi ya Abdilatif Abdalla, Sauti ya Dhiki (1973), Alamin Mazrui, Chembe cha Moyo (1988) na Said Ahmed Mohammed, Jicho la Ndani (2002)
    URI
    https://karuspace.karu.ac.ke/handle/20.500.12092/2243
    Collections
    • Department of Humanities and Languages [48]

    Karatina University copyright © 2017-2019  | Powered by DSpace
    Contact Us | Send Feedback | OAI-PMH Compliant
    Theme by Systems Librarian
      

     

    Browse

    All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Statistics

    View Usage Statistics

    Karatina University copyright © 2017-2019  | Powered by DSpace
    Contact Us | Send Feedback | OAI-PMH Compliant
    Theme by Systems Librarian