• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Research Publications
    • School of Education and Social sciences
    • Department of Humanities and Languages
    • View Item
    •   Repository Home
    • Research Publications
    • School of Education and Social sciences
    • Department of Humanities and Languages
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    FULLTEXT.pdf (276.6Kb)
    Date
    2022-08-08
    Author
    Ng’etich1*, Daniel Kiprugut
    Wafula1, Richard Makhanu
    Maitaria1, Joseph Nyehita
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    IKISIRI Makala hii inaangazia dhima ya maongezi katika riwaya ya Kiswahili. Riwaya ni mojawapo wa tanzu muhimu za fasihi ya Kiswahili ambayo inaendelea kukua kwa upande wa wahusika, dhamira, maudhui, mtindo na upeo. Utanzu wa riwaya ya Kiswahili ulianza mwanzo wa karne ya ishirini wakati James Juma Mbotela alipoandika riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934). Ukuaji wake umeshika kasi zaidi katika mwongo wa mwisho wa karne ya ishirini na mwanzo wa karne ya ishirini na moja. Ni muhimu pia kutambua kuwa, utungaji wa riwaya umeendelea kukua sambamba na uhakiki wake. Katika karne ya ishirini na moja, riwaya ya Kiswahili imefikia utungaji wa kimajaribio (Mwamzandi, 2013:48-66 na Mohamed 2003:78-79). Katika riwaya za kimajaribio, watunzi hujumuisha nadharia, visasili pamoja na kuzungumzia masuala ya utandawazi na soko huru. Ni riwaya ambazo hukiuka miundo ya riwaya iliyozoeleka. Kwa upande wa maongezi, usemaji wa wahusika katika riwaya umekua kutoka sahili hadi changamano kutokana na masuala yanayojadiliwa katika riwaya mahususi. Ni maoni ya waandishi wa makala hii kuwa, usemaji wa wahusika unaweza kuathirika na vipindi vya kihistoria hivyo basi kuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya riwaya. Madhumuni ya makala hii ilikuwa ni kuainisha maongezi katika riwaya za Kiswahili. Riwaya ambazo zilichanganuliwa kwa mujibu wa makala hii ni Kusadikika (1951), Mafuta (1984) na Kufa Kuzikana (2003). Riwaya hizo ziliteuliwa kuwakilisha vipindi mahususi vya ukuaji na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Usemi Hakiki. Kutokana na uchanganuzi huo, makala hii imebainisha mchango wa maongezi kwa ukuaji, maendeleo na uumbufu wa utanzu wa riwaya kwa ujumla.
    URI
    https://doi.org/10.37284/eajss.5.1.781
    https://karuspace.karu.ac.ke/handle/20.500.12092/2541
    Collections
    • Department of Humanities and Languages [48]

    Karatina University copyright © 2017-2019  | Powered by DSpace
    Contact Us | Send Feedback | OAI-PMH Compliant
    Theme by Systems Librarian
      

     

    Browse

    All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Statistics

    View Usage Statistics

    Karatina University copyright © 2017-2019  | Powered by DSpace
    Contact Us | Send Feedback | OAI-PMH Compliant
    Theme by Systems Librarian